Kikosi charejea, wachezaji wapewa mapumziko

Baada ya mchezo wa jana tulioibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Fountain Gate, kikosi chetu kimerejea jijini Dar es Salaam mchana huku wachezaji wakipewa mapumziko.

Kwa sasa tuko kwenye mapumziko ya Kalenda ya FIFA ambayo inaanza Oktoba 9-17, hivyo Ligi itasimama kupisha mechi za timu za taifa kwa hiyo katika kipindi hiki wachezaji watapumzika.

Wakati huo huo wchezaji walioitwa timu zao za taifa wameruhusiwa kwenda kujiunga nazo kutumikia mataifa yao.

Baada ya ratiba ya kalenda ya FIFA kumalizika kikosi kitarejea haraka kambini kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa African Football League dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Oktoba 20.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER