Kikosi charejea mazoezini kujiandaa na Azam

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya gym kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Januari Mosi.

Baada ya ushindi wa mabao 4-1 tuliopata dhidi ya KMC, Desemba 24 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora wachezaji walipewa mapumziko kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi kabla ya leo kurejea mazoezini.

Mazoezi ya gym husaidia kurejesha hali za utimamu wa mwili kwa wachezaji kabla ya kwenda uwanjani kujifunza mbinu mbalimbali.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo ikiwa ni hatua nzuri kwa benchi la ufundi kutoa mbinu kuelekea mechi dhidi ya Azam.

SHARE :
Facebook
Twitter

4 Responses

  1. Wazo langu, habari za huku angalau ziwe na details zaidi, maana bazooka huku ndo zipo kwenye page ya Instagram na zngne, angalau viwe vitu mbali mbali , hata habari za kuchangia uwanja sizioni zikiwa updated ♥ #nguvumoja One team ♥ one dream

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER