Kikosi chaanza safari kuelekea Morocco

Baada ya jana kushindwa kusafiri leo asubuhi kikosi chetu kimeanza safari ya kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Ijumaa, Machi 31.

Kikosi kilitakiwa kuondoka jana lakini Ndege tuliyokuwa tunasafiria ilipata hitilafu iliyofanya safari kushindwa kuendelea.

Timu inatarajia kufika leo jioni ambapo itapitia Qatar kabla ya kuunganisha hadi nchini Morocco.

Wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha Tanzania ‘Taifa Stars’ wao wataondoka mchana kuelekea Morocco kuungana na wenzao.

Kwa upande wa wale wa kimataifa watatokea kwenye mataifa yao na kuungana na timu ikiwa Morocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER