Simba Queens itashuka katika Uwanja wa Abebe Bikila saa tano asubuhi kuikabili Kawempe Muslim kutoka Uganda katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Kocha Juma Mgunda amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili kwenye kikosi cha leo ukilinganisha na kile kilichocheza mechi iliyopita dhidi ya FAD Djibouti.
Mgunda amewaanzisha Asha Djafar na Asha Rashid kuchukua nafasi za Amina Bilal na Ritticia Nabbosa ambao walianza mechi iliyopita.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Caroline Rufa (18), Fatuma Issa (5), Wincate Kaari (12), Ruth Ingosi (20), Violeth Nicholas (26), Vivian Corazone (17), Elizabeth Wambui (4), Precious Christopher (8), Jentrix Shikangwa (25), Asha Rashid (14), Asha Djafari (24).
Wachezaji wa Akiba:
Janeth Shija (1), Dotto Evarist (2), Esther Mayala (23), Daniela Ngoyi (22), Saiki Mary (19), Ritticia Nabbosa (13), Amina Bilali (11), Shelda Boniface (9).