Kikosi cha Queens kitakachotuwakilisha dhidi ya Mkwawa Leo

 

Kikosi chetu cha Simba Queens leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Chuo cha Mkwawa Mjini Iringa kuikabili Mkwawa Queens katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL).

Kocha Mkuu Charles Lukula amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu ukilinganisha na kikosi kilichocheza na Fountain Gate ambapo mlinda mlango Gelwa Yohan, Asha Juma na Dotto Evarist wameanza wakichukua nafasi za Janeth Shija, Daniela Ngoyi na Diana Mnali.

Nahodha Opa Clement ataendelea kuongoza mashambulizi sambamba na Asha Djafar na Jentrix Shikangwa.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Gelwa Yohan (21), Asha Juma (10), Dotto Evarist (11), Violeth Nicholas (26), Ruth Ingosi (20), Joelle Bukuru (18), Vivian Corazone (4), Pambani Kuzoya (17), Asha Djafar (24), Opa Clement (7), Jentrix Shikangwa (25).

Wachezaji wa Akiba

Zubeda Mohamed (29), Esther Mayala (23), Daniela Ngoyi (22), Koku Ally (19), Jackline Albert (16), Amina Hemed (14), Philomena Abakah (6), Olaiya Barakat (9) Zainabu Mohamed (8)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER