Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens leo itashuka katika Uwanja wa Azam Complex saa moja usiku kuikabili AS Kigali kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Queens itaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na lengo moja la kupambana kuhakikisha tunashinda na kutinga fainali baada kushinda mechi zote za hatua ya makundi.
Kikosi Kamili Kilivyopangwa
Zubeda mgunda (29), Diana William (15), Fatuma Issa (5), Esther Mayala (23), Daniella Kanyanya (22), Vivian Corazone (4), Philomena Abakah (27), Joelle Bukuru (18), Opa Clement (7), Aisha Juma (10), Asha Djafari (24).
Wachezaji wa Akiba
Gelwa yonah (21), Doto Evarist (11), Violeth Nicholaus (26), Silvia Thomas (12), Sarrive Badiambila (2), Olaiya Barakat (9), Topister Situma (13), Pambani Kuzoya (17)
Amina Ramadhani (14).