Mlinzi mpya, Kelvin Kijili amesema ndoto yake ilikuwa kucheza kwenye kikosi chetu tangu akiwa mtoto na leo imetimia rasmi.
Kijili ameyasema hayo muda mfupi baada ya kujiunga kambini na wenzake nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.
Kijili amesema alikuwa ana ndoto za kucheza Simba na Leo imetimia na atahakikisha anajitoa kwa kila kitu ili kuwafurahisha mashabiki.
Kijili amewaahidi mashabiki atapambana muda wote kwa ajili ya kuwafurahisha pamoja na kuisaidia timu kupata matokeo chanya akisaidiana na wachezaji wenzake.
“Nimefurahi kuwa hapa, hii ni ndoto yangu ambayo nilikuwa nao tangu nikiwa mtoto na leo imetimia. Simba ni Klabu ya ndoto yangu na nitahakikisha naisadia kufanya vizuri.”
“Mashabiki wetu naomba mnipe ushirikiano mkubwa nami nitahakikisha nawalipa furaha uwanjani,” amesema Kijili.