Kibu mchezaji bora Mei

Kiungo mshambuliaji, Kibu Denis amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Mei (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Kibu ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwapiku viungo Rally Bwalya pamoja na Mzamiru Yassin.

Katika mwezi Mei, Kibu amecheza mechi saba sawa na dakika 630 akifunga mabao matano na kusaidia kupatikana kwa bao moja.

Kwa kushinda kinyang’anyiro hicho Kibu atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Mchanganuo wa kura

Jina Kura Asilimia

Kibu 474 84

Bwalya 67 11

Mzamiru 19 3

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER