Kibu kwa mara ya kwanza michuano ya Afrika Leo

Mshambuliaji Kibu Denis ameanza kwenye kikosi chetu kitakacho tuwakilisha dhidi ya RS Berkane ikiwa ni mara ya kwanza kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika tangu ajiunge nasi.

Kibu alijiunga nasi akitokea Mbeya City mwanzoni mwa msimu lakini usajili wake wa Shirikisho la soka Afrika CAF ulichelewa na leo ndio mara yake ya kwanza.

Kibu ataongoza mashambulizi pamoja na Medie Kagere ambapo watapata msaada wa karibu kutoka Rally Bwalya na Pape Sakho.

Mbali na Kibu kocha Pablo Franco amefanya mabadiliko mengine mawili ya wachezaji ambao hawakuwepo katika kikosi kilichocheza mechi ya kwanza nchini Morocco.

Wachezaji hao ni Jonas Mkude aliyekuwa majeruhi na Bwalya ambaye alienda nchini kwao Zambia kwa mambo ya kifamilia.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (17), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38), Rally Bwalya (8).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Thadeo Lwanga (4), Bernard Morrison (3), Mzamiru Yassin (19), Chris Mugalu (7), Peter Banda (11).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER