Kibu, Kagere kuiongoza Simba dhidi ya Polisi Tanzania

Washambuliaji Kibu Denis na Medie Kagere wataongoza idara yetu ya ushambuliaji katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mchezo wa leo utakuwa ni wa kwanza wa kimashindano kwa Kibu akiwa na jezi yetu msimu huu tangu alipojiunga nasi.

Kibu na Kagere watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Rally Bwalya na Hassan Dilunga.

Mlinzi wa kati Joash Onyango amerejea kikosini kuchukua nafasi ya Pascal Wawa ambapo atacheza sambamba na Henock Inonga.

Kiraka Erasto Nyoni amepangwa kama kiungo wa ulinzi akichukua nafasi ya Taddeo Lwanga ambapo atacheza pamoja na Sadio Kanoute.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Erasto Nyoni (18), Kibu Denis (38), Sadio Kanoute (13), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Hassan Dilunga (24).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5) Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Peter Banda (11) Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Duncan Nyoni (23), Bernard Morrison (3).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER