Nyota wetu watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa mwezi Mei wa mashabiki (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Wachezaji hao ni viungo washambuliaji Kibu Denis na Rally Bwalya pamoja na kiungo mkabaji Mzamiru Yassin.
Walinzi wa kati Henock Inonga na Joash Onyango waliingia tano bora lakini baada ya kuchujwa wamebaki nyota hao watatu waliotinga fainali.
Mchanganuo wa takwimu zao za mwezi Mei.
Mechi dakika Goli Assist
- Kibu 7 630 5 1
- Bwalya 7 508 1 4
- Mzamiru 6 465 0 0
Zoezi la kupiga kura kwa mashabiki tayari limeanza kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litakamilika Juni Mosi saa sita usiku.
Mshindi wa jumla atakabidhiwa kitita cha Sh.2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.
5 Responses
Nguvu moja
Kibu denis
Nampigia kura kibu denis,kuwa mchezaji bora wa mwezi mei
Kibu Denis Prospa
Kibu denis anastahili kwa mchango wake kwenye mechi alizocheza