Kibu aahidi makubwa Simba

Baada ya suala lake la vibali kutoka serikalini kukamilika mshambuliaji wetu Kibu Denis ameahidi kujitoa hadi jasho la mwisho kuhakikisha Simba inapata mafanikio.

Kibu amesema baada ya klabu kumuamini na kumsajili anajiona ana deni kubwa na kuahidi atalipa kwa kuisaidia timu uwanjani kila atakapopata nafasi.

Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri hivyo ili kupata nafasi ya kucheza unapaswa kujituma kulishawishi benchi la ufundi.

“Wanasimba wasubiri tu mambo mazuri yanakuja, wameonyesha imani kubwa kwangu nami nitawalipa uwanjani hiyo ndiyo ahadi yangu kwao,” amesema Kibu.

Kibu yupo nchini Benin na kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachojiandaa na mchezo wa marudiano wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia utakaopigwa kesho jioni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER