Kennedy, Sakho wawekwa chini ya uangalizi, waendelea vizuri

Mlinzi wa kati Kennedy Juma na kiungo mshambuliaji Pape Sakho wanaendelea vizuri baada ya kupelekwa hospitali kutokana na kuumia kwenye mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji.

Sakho aliumia mapema dakika ya 10 na kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kukanyagwa kwa nyuma na mlinzi wa Dodoma wakati Kennedy alipigwa kiwiko chini ya jicho na mshambuliaji Anuary Jabir dakika ya 43 na kutolewa.

Baada ya kupata vipimo vya daktari wawili hao wameonekana wanaendelea vizuri na watapewa mapumziko ya siku chache wakiwa chini ya uangalizi kabla ya kurejea mazoezini.

Kiungo mkabaji Taddeo Lwanga ambaye pia alishindwa kuendelea na mchezo kipindi cha pili yeye alipata maumivu kidogo na alitibiwa pale pale uwanjani na yuko fiti kwa sasa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER