Kennedy, Israel wajiunga na timu Zanzibar

Wachezaji Kennedy Juma na Israel Patrick wamejiunga na kikosi baada ya kurejea kutoka katika kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilichosafiri jana kuelekea Misri kwa ajili ya kambi.

Wawili hao walikuwa katika kikosi cha awali cha Stars kilichoitwa kwa ajili ya michuano ya AFCON lakini baada ya mchujo hawakujumuishwa hivyo wamejiunga na timu.

Kennedy na Israel wameshiriki katika mazoezi ya mwisho ya kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Singida Fountain Gate yaliyofanyika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex.

Kennedy na Israel wanakifanya kikosi chetu kiwe na wachezaji 22 ambao tutawatumia kwa ajili ya michuano hii ya Mapinduzi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER