Mlinzi wa kati Kennedy Juma ametoboa siri ya kiwango chake kuimarika ni mazoezi, kujituma, kujitunza na kujitambua kuwa ni mchezaji na muda wowote akipewa nafasi ya kucheza.
Kennedy amesema ukipewa nafasi hiyo unakuwa umechagua mpira uwe ndiyo kazi yako unapaswa kuhakikisha unajituma na kujitunza ili kuhakikisha unafanya vizuri na kuwafanya waliokupa nafasi hiyo wazidi kukuamini.
Mlinzi huyo ameongeza kuwa ingawa hatujapata matokeo ya ushindi katika mechi zetu tatu zilizopita ikiwemo ya Tamasha la Simba Day dhidi ya TP Mazembe kuwa huwa inatokea kwenye mpira na anaamini tutarejea katika makali yetu.
“Hatujapata ushindi kwenye mechi kadhaa zilizopita lakini sisi bado ni bora wachezaji wanaendelea kuzoeana na tutarudi kwenye ubora wetu na kuendelea kushinda kama kawaida,” amesema Kennedy.
Kuhusu nyota wapya tuliowasajili Kennedy amesema ni wachezaji wazuri na watakuwa msaada mkubwa kwa timu katika siku za usoni hivyo amewaomba mashabiki waendelee kuwapa muda na wasiwavunje moyo