Tumefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi wa kulia Kelvin Kijili kutoka Singida Fountain Gate kwa mkataba wa miaka miwili.
Kijili mwenye umri wa miaka 24 ni kijana mwenye kipaji na kasi na amekuwa akitumika kuanzisha mashambulizi kutokea upande wa kulia.
Akiwa na Singida Fountain Gate msimu uliopita Kijili amesaidia kupatikana kwa mabao manne (assist).
Kijili amekuja kuongeza kitu kikubwa kwenye kikosi chetu na kutokana na umri alionao tunaamini ataendelea kuwa msaada kwa timu kwa muda mrefu.
Usajili tuliofanya kuelekea msimu mpya wa mashindano tumezingatia kigezo cha umri kwakuwa malengo yetu ni kujenga timu imara ya muda mrefu.
Tayari Kijili amejiunga na wenzake kambini nchini Misri kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2024/25.