Uzinduzi wa kampeni kampeni ya hamasa kuelekea mchezo wetu wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco utakaofanyika Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa umefanyika katika Tawi la Home Boys, Wazo Hill Tegeta.
Viongozi mbalimbali wamejitokeza na kutoa kauli za hamasa kuelekea mchezo huo mkubwa.
Mwenyekiti Murtaza Mangungu
Maandalizi yote yanayotakiwa kufanyika ndani na nje ya uwanja yamefanyika, lengo letu ni kuhakikisha mashabiki wanaujaza uwanja wote wa Benjamin Mkapa.
Sio mara ya kwanza kucheza mechi kubwa kama hii, wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo huu. Ilitokea bahati mbaya tutakapoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Horoya ugenini hilo hatutaki lijirudie tena.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Asha Baraka
Tuwe kitu kimoja tuungane katika mchezo wa Jumamosi kuifunga Raja, Iwe jua iwe mvua ushindi lazima. Hakuna kitu kingine tunahitaji zaidi ya ushindi.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Seleman Haroub
Ndio wiki ya kuonyesha Afrika kama Simba ni kitu gani, tudhihirishe Afrika kuwa Simba ni timu kubwa.
Kwa Mkapa Al Ahly amelala, Berkane amelala AS Vita vile vile nao Raja anatakiwa kulala kikubwa mashabiki mjitokeze kwa wingi.
Meneja Habari na Mawalisiano, Ahmed Ally
Ili tuweze kumfunga Raja uwepo wenu mashabiki ni muhimu, tutakuwa na Jukwaa Maalum la kushangilia pale chini ya TV Kubwa uwanjani ambalo linaitwa Mwanzo mwisho. Kama huwezi kungalia kuanzia mwanzo hadi mwisho tafuta sehemu nyingine ya kukaa.
Jumamosi matawi yote ya Simba yatakaa sehemu moja nyuma ya TV kubwa kwa ajili ya kushangilia. Nunua tiketi yako mapema ili kuepeuka usumbufu.
Jumamosi Raja atake asitake atatueleza alipoificha, tunataka kuwalipia kisasi wale waliofungwa mabao 6-0 mwaka 1998 na Wana Afrika wenzetu Vipers waliofungwa mabao 5-0.
Tunazo jezi nyingi lakini Mwanasimba hakikisha unavaa jezi nyekundu.