Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ihefu FC utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex saa 10 jioni.
Robertinho amesema ni mchezo muhimu ambao tunapaswa kushinda ili tuingie hatua ya nusu fainali na kila mmoja ndani ya timu analifahamu hilo.
Robertinho ameendelea kusema “tunahitaji kucheza vizuri na kupata ushindi utakaotupeleka nusu fainali. Tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu lakini tumejipanga.”
“Tumetoka kucheza mechi ngumu ya Ligi ya Mabingwa lakini hii pia ni muhimu kwetu tunahitaji kucheza vizuri tukiwa na mpira na tusipokuwa nao na kupata ushindi,” amesema Robertinho.
Robertinho amewaomba mashabiki kujitojeza kwa wingi uwanjani kesho kuipa sapoti timu kwakuwa wana mchango mkubwa kwa timu kupata ushindi.
“Mashabiki ni muhimu katika mchezo wa mpira, uwepo wao uwanjani unaongeza chachu na hamasa kwa wachezaji, tunawaomba waje kwa wingi kesho, tuna mchezo muhimu,” amesema Robertinho.