Kauli ya Robertinho kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Kesho

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema malengo yetu kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar ni kucheza soka safi na kupata ushindi.

Robertinho amesema timu yetu ipo kwenye viwango vya juu kwa mujibu wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) hivyo tunapaswa kulionyesha hilo uwanjani.

Hata hivyo Robertinho amesema anategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa na tunawaheshimu kama ambavyo wanapaswa kufanya hivyo kwetu.

“Tunahitaji kucheza soka safi na kushinda, hilo ndilo lengo letu. Simba ni timu kubwa na ipo juu kwenye viwango vya ubora wa Afrika, wapinzani wetu wanapaswa kutuheshimu nasi tunawaheshimu pia,” Robertinho, kocha mkuu.

Kwa upande wake mlinzi wa kulia, Israel Patrick amesema utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Mtibwa lakini tupo tayari kupambana huku akiwaomba mashabiki wajitojeze kwa wingi uwanjani.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Mtibwa ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Tunaomba mashabiki wetu mje kwa wingi uwanjani kutupa sapoti,” amesema Israel.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER