Kauli ya Robertinho baada ya ushindi dhidi ya Polisi

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema ushindi mnono wa mabao 6-1 tuliopata jana dhidi ya Polisi Tanzania ni sehemu ya kuandaa umbo zuri la kikosi kuelekea msimu ujao wa Ligi 2023/24.

Robertinho amesema ushindi katika mechi hizi za mwisho zina umuhimu mkubwa kwakuwa msimu mpya hauko mbali hivyo ni vema kuwajengea wachezaji hali ya kujiamini.

Robertinho pia amewapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliofanya ya kuhakikisha tunacheza vizuri na kupata ushindi mnono.

Aidha Robertinho amempongeza binafsi Saido Ntibazonkiza kwa kufunga mabao matano kwenye mchezo wa jana nakuwa miongoni mwa wanaogombania kwa karibu ufungaji bora.

“Nimefurahi kupata ushindi huu kwakuwa unatujengea umbo zuri kuelekea msimu mpya wa ligi. Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyofanya.

“Pia nampongeza Saido kwa kufunga mabao matano peke yake, sio jambo dogo anastahili pongezi,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER