Kauli ya Pablo kuelekea mechi dhidi ya Berkane

Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakuwa mgumu zaidi ya ule wa US Gendarmerie.

Pablo amesema wenyeji Berkane wametoka kupoteza mchezo uliopita ugenini hivyo watajipanga kuhakikisha wanafanya kila kitu ili kuwafurahisha mashabiki wao kwa kupata ushindi uwanja wa nyumbani.

Hata hivyo Pablo amesema hatupaswi kuhofia chochote badala yake amewataka wachezaji kupambana muda wote ili kutetea timu na kupata matokeo mazuri.

Pablo ameongeza kuwa tutawakosa baadhi ya wachezaji katika mchezo wa kesho kutokana na majeruhi huku wengine wakiwa wagonjwa.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Berkane wataingia kutafuta ushindi ili kuwafurahisha mashabiki wao. Na kwa upande wetu tutawakosa baadhi ya wachezaji lakini waliopo wanapaswa kuhakikisha wanapambana kwa ajili ya timu,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER