Kauli ya Pablo kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kagera

Kocha Mkuu Pablo Franco ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho wa Ligi kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakuwa ngumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu.

Pablo amesema hatua ilipofikia ligi kila mchezo unakuwa mgumu na kila timu inahitaji pointi tatu ili kujiweka vizuri katika msimamo.

Pablo ameongeza kuwa ingawa tutakosa baadhi ya wachezaji wetu wa kikosi cha kwanza kutokana na majeruhi lakini tutahakikisha tunashinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Mchezo utakuwa mgumu, Kagera ni timu nzuri na tunakumbuka walitufunga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ingawa nasi tulipoteza nafasi nyingi za kufunga.

“Tunahitaji kuwapa furaha mashabiki ambao mara zote wamekuwa nasi katika nyakati za furaha na huzuni. Tutawakosa baadhi ya wachezaji wetu muhimu kutokana na kuwa majeruhi lakini waliopo wapo tayari kupambana,” amesema Pablo.

Akizungumzia changamoto ya kufungwa mara kadhaa kwa mipira ya kutengwa Pablo amesema wanaendelea kuifanyia kazi mazoezini na kadiri muda unavyokwenda ndivyo inavyopungua.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER