Kauli ya Mgunda kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Singida

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigiwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Liti yamekamilika.

Mgunda amesema wachezaji wote waliosafiri wako kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao malengo yetu ni kuhakikisha tunapata alama tatu ugenini.

Mgunda ameongeza kuwa anaamini mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani hasa wanapokuwa nyumbani lakini tumejiandaa kikamilifu kufanya vizuri.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, tayari tumefika mkoani Singida wachezaji wako kwenye hali nzuri, tunaamini itakuwa mechi ngumu na tutapata upinzani mkubwa,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema ingawa tutakutana na timu ngumu lakini tupo tayari kuhakikisha tunapambana kushinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu.

“Simba ni timu kubwa na tunajua tunaenda kukutana na timu imara kwa hiyo tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER