Kauli ya Mgunda kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya City

 

Kocha Msaidizi Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa kesho saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, yamekamilika.

Mgunda amesema wachezaji wote wamerejea salama jijini Dar es salaam kutoka Dubai walikokuwa katika kambi ya siku nane na wako kwenye hali nzuri kupambania alama tatu.

Amesema tutaingia katika mchezo wa kesho kwa lengo moja tu la kuhakikisha tunabakisha pointi tatu nyumbani.

“Ligi ni ngumu hasa kipindi hiki inapoelekea ukingoni hivyo tutaingia katika mchezo huo kwa kuchukua tahadhari zote ili tufanikishe lengo letu.

“Tunaiheshimu Mbeya City ni timu nzuri lakini tupo tayari kupambana kwa ajili ya pointi tatu,” amesema Mgunda.

Katika mchezo wa kesho tutaendelea kukosa huduma ya Moses Phiri na Peter Banda ambao wamerejea mazoezini lakini hawana utimamu wa asilimia 100.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER