Kauli ya Mgunda kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya KMC

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC yamekamilika na wachezaji wapo tayari kwa mpambano.

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na leo watafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kushuka katika Uwanja wa CCM Kirumba kuikabili KMC.

Mgunda ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu KMC, tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunashinda na kuchukua alama zote tatu.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, kikosi kipo tayari kuwakabili KMC, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Mgunda.

Kocha Mgunda amesema katika mchezo wa kesho tutawakosa huduma ya mshambuliaji Moses Phiri kutokana na kupata majeraha kwenye mechi iliyopita ingawa anaendelea vizuri kwa sasa.

“Phiri hatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho, kama mnavyofahamu aliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar lakini sasa anaendelea vizuri,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER