Kauli ya Mgunda baada ya ushindi dhidi ya Polisi

 

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema baada ya ushindi wa mabao 3-1 tuliopata mbele ya Polisi Tanzania sasa tunaelekeza nguvu katika mechi inayofuata dhidi ya Coastal Union.

Mgunda amesema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa leo yatafanyiwa kazi mazoezini kabla ya mechi ijayo.

Mgunda ameongeza kuwa ingawa tumefanikiwa kupata ushindi lakini Polisi wametupa upinzani mkubwa kitu ambacho tunategemea kutokea katika mchezo ujao.

“Mechi dhidi ya Polisi imemalizika sasa tunajiandaa na mchezo ujao. Ulikuwa mchezo mzuri wenye upinzani mkubwa na tushukuru Mungu tumefanikiwa kupata ushindi mnono ugenini.

“Pamoja na ushindi tuliopata lakini kuna mapungufu yameonekana na mimi kama mwalimu na benchi langu la ufundi tutayafanyia kazi mazoezini ili mchezo ujao yasiwepo,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER