Kauli ya Matola kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Jamhuri

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa robo fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:15 usiku.

Matola amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu.

Matola ameongeza kuwa Jamhuri haikufika hatua hiyo kwa kubahatisha bali imepambana kwahiyo haiwezi kuwa mechi rahisi kesho.

“Haitakuwa mechi rahisi, Jamhuri ni timu bora na haikufika hatua hii kwa bahati mbaya imepambana, tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga.”

“Kwa upande wetu tumejiandaa vizuri, wachezaji wapo kwenye hali nzuri lengo letu ni kuhakikisha tunashinda na kuingia nusu fainali,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER