Mwenyekiti wa Klabu ya Simba upande wa Wanachama, Murtza Mangungu amesema bado hatujamaliza kufanya usajili wa wachezaji wapya kwenye kikosi chetu.
Mangungu amesema wiki hii tutambulisha wachezaji wengine ambao watatikisa nchi na kivutio kwenye kilele cha Simba Day Agosti 8.
Mangungu amesema uzinduzi wa jezi zetu bora za msimu huu ambazo hazina makorokoro zitanduliwa wiki hii.
“Niwaibie siri tu kuwa hatujamliza usajili kuna vyuma bado havijatambulishwa. Msimu huu tumejipanga na Wanasimba wenzangu tuko vizuri sana.
“Jezi bora itazinduliwa wiki haina makorokoro wala majumba ya makumbusho ni jezi ambayo itaweka historian,” amesema Mangungu.