Kauli ya Kocha Zoran baada ya ushindi dhidi ya Geita

Kocha Mkuu Zoran Maki, amewasifu wachezaji kwa mchezo mzuri kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold tulioupata jana katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC.

Kocha Zoran amewasifu nyota wetu kutokana na kucheza vizuri baada ya kutoka kucheza mchezo mkubwa wa Ngao ya Jamii ndani ya siku tatu.

Zoran ameongeza kuwa wachezaji wamewahi kurudi katika hali ya kawaida na kupambana kupata ushindi mnono wa mabao matatu kwenye mechi ngumu ya Geita.

“Kwanza nawapongeza wachezaji wangu kwa kucheza vizuri na kupata ushindi mnono wa mabao matatu. Haikuwa kazi rahisi mechi ilikuwa ngumu.

“Tumetoka kucheza mechi kubwa na tumecheza ndani ya siku tatu, si kitu kidogo na imetupa mwanzo mzuri wa ligi na wachezaji wanaendelea kuzoeana,” amesema kocha Zoran.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER