Kauli ya Kocha Pablo kuhusu mchezo na Namungo

Kocha Mkuu Pablo Franco, amefunguka kuwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo utakaopigwa uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utakuwa mgumu kwetu kutokana na kukosa maandalizi mazuri.

Pablo amesema baada ya mchezo wa Derby Jumapili wachezaji hawajapata muda wa kufanya mazoezi zaidi ya utimamu wa mwili kabla ya kuanza safari.

Pablo ameongeza mchezo utakuwa mgumu na anaikumbuka mechi ya mwisho tuliyokutana na Namungo katika michuano ya Mapinduzi ilivyokuwa na ushindani licha ya kuibuka na ushindi.

“Nadhani mchezo utakuwa mgumu zaidi kwetu sababu hatujapata muda wa maandalizi. Tumetoka kucheza mechi kubwa ya Derby na hapo hapo tukatakiwa kusafiri kuja huku.

“Naikumbuka vizuri Namungo katika michuano ya Mapinduzi, tuliwafunga mabao 2-1 lakini mechi ilikuwa ngumu na ushindani mkubwa. Sisi ni Simba tutajitahidi kutafuta alama tatu,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER