Kauli ya Kocha Mgunda kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Namungo

Kocha Mkuu Juma Mgunda, amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC yamekamilika na lengo letu ni kuhakikisha tunapata alama tatu.

Mgunda amesema ligi inavyozidi kusonga ugumu unazidi kuongezeka na kila timu tunayokutana nayo inakuwa imejipanga kutafuta alama tatu.

Kuhusu mbio za ubingwa Mgunda amesema tutaendelea kupambana hadi siku ya mwisho na hatuwezi kukata tamaa ingawa ligi ni ngumu.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, bado tuna changamoto ya majeruhi lakini wachezaji walio fiti wapo tayari kwa mechi ya kesho. Tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tupo tayari kuwakabili Namungo,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake mlinda mlango, Ally Salim amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kutupa sapoti kwakuwa tunawategemea kuhakikisha tunapata ushindi.

“Mashabiki ni watu muhimu tunawahitaji kwenye mchezo wa kesho, tunajua utakuwa mgumu lakini tupo tayari kupambana,” amesema Salim.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER