Kauli ya Kocha Matola kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Singida FG

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa kesho saa 2:15 usiku Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Matola amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri morali ipo juu na kila mchezaji anajua umuhimu wa ushindi kwenye mchezo wa kesho.

Matola amesema tunawaheshimu Singida kutokana na ubora walionao na tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Timu iko tayari kwa mchezo wa kesho, wachezaji wapo kwenye hali nzuri na maandalizi yanaendelea.

“Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Singida lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunapata ushindi na kuchukua pointi zote tatu nyumbani,” amesema Matola.

Tunaingia kwenye mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-1 tuliopata Jumamosi dhidi ya Coastal Union.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER