Kauli ya Kocha Matola kuelekea mchezo dhidi ya Prisons

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Matola amesema mara zote tunapokutana na Prisons mchezo unakuwa mgumu na kwa sasa wapo kwenye kiwango bora lakini tumejipanga kuwakabili.

Akizungumzia kikosi chetu Matola amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wapo tayari kwa mtanange ambao lengo ni kuhakikisha tunapata ushindi.

“Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Prisons, mara zote tunapokutana inakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Matola.

Matola ameongeza kuwa kiungo mkabaji Sadio Kanoute hatakuwa sehemu ya kikosi kutokana na kuendelea kuuguza majeraha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER