Kauli ya Kocha Matola kuelekea mchezo dhidi ya Namungo

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo utakaopigwa kesho saa 12 jioni katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Mkoani Lindi utakuwa mgumu.

Matola amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani pia Ligi inaelekea ukingoni kwahiyo kila timu inajipanga kuhakikisha inakusanya pointi nyingi hasa kwenye Uwanja wa nyumbani.

Matola amesema tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo tunafahamu tunaenda kukutana na timu imara lakini tupo tayari kuwakabili na kuchukua pointi zote tatu.

“Utakuwa mchezo mgumu, Namungo ina timu imara yenye wachezaji wazoefu, kwahiyo tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejidhatiti kwa ajili ya kupata ushindi,” amesema Matola.

Kocha Matola pia ameweka wazi kuwa katika mchezo wa kesho tutawakosa nyota wetu watano ambao ni Henock Inonga, Shomari Kapombe, Clatous Chama, Luis Miqussone, Ladaki Chasambi ambao ni majeruhi huku Sadio Kanoute yeye akiangaliwa hali yake baada ya mazoezi ya mwisho leo jioni.

Akiongeza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia Israel Patrick amesema “tupo tayari kupambana kuhakikisha tubaisaidia timu kupata matokeo mazuri na kuwapa furaha Wanasimba.”

“Haitakuwa mechi rahisi hata kidogo, Namungo ni timu nzuri lakini tumejiandaa kuwakabili na kufuata maelekezo tutakayopewa na walimu,” amesema Israel.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER