Kauli ya Kocha Gomez kuelekea mchezo dhidi ya Tanzania Prisons

Kocha Mkuu, Didier Gomez amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kesho Jumatano Machi 10, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Kocha Gomez amesema anaiheshimu Prisons ana anafahamu kuwa ilitufunga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza hivyo amekiandaa kikosi kuhakikisha tunapata ushindi.

Gomez ameongeza kuwa ushindi kwenye mchezo wa kesho utapunguza idadi ya alama kufikia mbili dhidi ya wanaongoza ligi huku bado tukiwa na michezo mitatu mkononi.

“Kikosi kipo tayari kwa mchezo wa kesho, wachezaji wamefanya mazoezi jioni ya leo wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu. Tunahitaji alama tatu za kesho ili kupunguza idadi ya alama na kuwapa presha wanaongoza,” amesema Kocha Gomez.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Dear Coach

    Greetings

    Hopefully your doing good on this smart timezone I’m Simba sc fun since young age simba is my favourite time forever .
    All be best for today’s game but how was this MANURA know his health is good ?
    I wish all the best Allah will bless him.
    Regards:
    Mursal Maulid Mahayu
    mahayumursal@gmail.com
    +255 765 480 905
    Dar es salaam “kigamboni” Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER