Kauli ya Kocha Gomez baada ya ushindi dhidi ya Kagera Sugar

Baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup kwa kuifunga Kagera Sugar mabao 2-1, Kocha Mkuu Didier Gomez amesema malengo yetu yetu ya kutetea taji hilo yanaelekea kufanikiwa.

Gomez amesema tunahitaji kutetea ubingwa wa michuano hiyo ili kuonyesha tofauti na timu nyingine na kudhihirisha uwezo mkubwa tulio nao.

Akizungumzia mchezo wenyewe Kocha Gomez amewasifu wachezaji kutokana na uwezo walioonyesha kutoka nyuma na kusawazisha kabla ya kupata bao la ushindi.

“Tumemiliki sehemu kubwa ya mchezo, kipindi cha kwanza tulicheza vizuri lakini hatukupata bahati ya kufunga. Kipindi cha pili niliwaingiza Bernard Morrison na John Bocco kwa ajili ya kuongeza kasi kwenye ushambuliaji na tulifanikiwa,” amesema Gomez.

Kocha Gomez pia ameuzungumzia mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Watani wa jadi Yanga kuwa ni muhimu kushinda kwa kuwa unaamua mustakabali wa ubingwa msimu huu.

“Kuelekea mchezo dhidi ya Yanga sisi morali yetu ipo juu, tumetoka kucheza mechi sita na kushinda zote na mechi hii itaonyesha nani atakuwa bingwa kwa hiyo ni vizuri kushinda nayo,” amesema Gomez.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER