Kocha Mkuu, Didier Gomez amefurahishwa na uwezo ulioonyeshwa na wachezaji wetu uliofanikisha ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita na kutufanya kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa tukiwa vinara wa Kundi A.
Gomez amesema wachezaji wote walicheza vizuri na kutimiza majukumu yao huku akisisitiza kuwa tulistahili kupata ushindi mnono zaidi kutokana na nafasi tulizotengeneza.
Raia huyo wa Ufaransa ameongeza kuwa jambo la muhimu ni kufuzu robo fainali ya michuano hiyo kwa kumaliza tukiwa vinara juu ya Al Ahly na Vita kitu ambapo haikuwa kazi rahisi.
“Nimefuraishwa na ushindi huu mnono ingawa tulistahili kupata mabao mengi zaidi, kumaliza tukiwa kinara mbele ya Al Ahly na Vita ni kitu cha kuvutia zaidi,” amesema Kocha Gomez.
Kuelekea mchezo Al Ahly utakaopigwa Aprili 9 nchini Misri Kocha Gomez amesema imebaki wiki moja ya kufanya maandalizi ila kwa sasa ni muda wa kufurahi kwa ushindi uliopatikana.
Matokeo yoyote yatakayopatikana kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Al Ahly hayataathiri msimamo wa kundi letu.
2 Responses
Nguvu moja
All the best to us!
But let’s see the full fixtures with categories of the competition