Kauli ya Kocha Fadlu kuelekea mchezo dhidi ya Fountain Gate

Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate FC yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri.

Kocha Fadlu amesema kikosi chetu kinaendelea kupata muunganiko mzuri na sasa timu inatengeneza nafasi kuanzia nyuma katika idara ya ulinzi mpaka ushambuliaji.

Fadlu ameongeza kuwa kama tungekuwa makini katika mchezo uliopita dhidi ya Tabora United tulikuwa tunaweza kupata ushindi mnono zaidi ya mabao matatu tuliyofunga.

“Kikosi kinazidi kuimarika siku hadi siku, timu ipo kwenye umbo zuri. Tunatengeneza mashambulizi kuanzia nyuma kwenda mbele na maelewano ni makubwa.”

Kwa upande wake nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema kwa upande wao kama wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo ya walimu ili kuisaidia timu kupata matokeo chanya.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, Fountain Gate wana timu imara lakini tumejipanga na tupo tayari kuwakabili na tutafuata maelekezo tutakayopewa na

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER