Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga yamekamilika na kila kitu kipo sawa.
Fadlu amesema tumepata nafasi nzuri ya kufanya maandalizi kuelekea mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu lakini tupo tayari kuhakikisha tunapata alama tatu.
Akizungumzia hali ya kilosi, Kocha Fadlu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na tupo tayari kuonyesha soka safi na kupata matokeo chanya.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunafahamu utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kufanya vizuri. Yanga ni timu bora na itatupa ushindani mkubwa lakini tupo tumejiandaa,” amesema Fadlu.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia Shomari Kapombe amesema kwa upande wao wapo kamili kuipigania timu kupata ushindi ili kuwapa furaha Wanasimba.
“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kupambana hadi mwisho na kufuata maelekezo ya walimu wetu lengo likiwa kuwapa furaha Wanasimba,” amesema Kapombe.