Kauli ya Kocha Cadena kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold

Kocha wa Makipa, Daniel Cadena amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold utakaopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba saa 10 jioni.

Cadena amesema utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia tupo kwenye mbio za ubingwa lakini wachezaji wote wapo timamu asilimia 100 kupambana hadi mwisho na kupata ushindi.

Cadena ameongeza kuwa ratiba ni ngumu kutokana na kucheza mechi kila baada ya siku mbili huku tukikosa muda mzuri wa kufanya mazoezi lakini hata hivyo tupo kamili kupambana na changamoto zote ili tupate ushindi.

“Kwa upande wetu tupo tayari kwa mchezo wa kesho, haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa wapinzani na jambo jema ni kwamba hatuna mchezaji majeruhi,” amesema Cadena.

Mlinzi wa kati Hussein Kazi akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema kwa sasa kila mchezo kwetu ni fainali na tutaingia katika mechi ya kesho kwa lengo la kuzisaka pointi tatu muhimu.

Kazi ambaye msimu uliopita alikuwa mchezaji wa Geita amesema tutaingia kwa kuwaheshimu Geita tunajua tutapata upinzani mkubwa lakini tupo tayari kwa kila kitu ili tufanikiwe kupata ushindi.

“Ligi ni ngumu, kwetu kila mchezo ni fainali. Bado tupo kwenye kupigania ubingwa mechi bado ziko nyingi na tunaanza kesho dhidi ya Geita,” amesema Kazi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER