Kauli ya Kocha Benchikha kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya ASEC

Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha amesema malengo yetu kwenye mchezo wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ni kupambana ili kupata ushindi.

Benchikha amesema utakuwa mchezo mgumu hasa kwakuwa tunacheza ugenini lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi.

Aidha Benchikha ameongeza kuwa wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wapo tayari kwa ajili ya kupambana.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, tunahitaji kushinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya robo fainali, malengo yetu ni kupata pointi tatu,” amesema Benchikha.

Kwa upande wake mshambuliaji, Freddy Michael Kouablan amesema anajisikia fahari kucheza katika ardhi ya nyumbani kwao Ivory Coast kwakuwa familia na ndugu zake watakuja uwanjani kumtazama.

“Inafurahisha kucheza katika ardhi ya nyumbani, ndugu pamoja na familia wanakuja uwanjani kukupa sapoti. Sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana ili kuisaidia timu kupata ushindi,” amesema Freddy.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER