Kauli ya Chama baada ya kukabidhiwa tuzo ya Emirate

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama amewashukuru wote waliomuwezesha kupata tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Chama ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya pili msimu huu baada ya kuwashinda Nahodha John Bocco na Shomari Kapombe ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

“Kwanza namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika hapa, naishukuru familia yangu kwa kunitia moyo, nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa uwanjani na mashabiki walionipigia kura.

“Tuzo hii inaongeza hamasa kwa wachezaji ya kuipambania timu, kila mmoja anafanya jitihada za kuipata na hilo ni jambo zuri kwa timu,” amesema Chama.

Chama ameongeza kuwa; “ni mara ya pili msimu huu kuchukua tuzo hii, lengo langu ni kuchukua tena na tena kwakuwa mpira ndio kazi yangu na nipo hapa kuisaidia Simba.”

Chama amekabidhiwa tuzo na pesa taslimu Sh. 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

Katika mwezi Desemba, Chama amecheza dakika 540 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine saba (assist).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER