Tumefanikiwa kuinasa saini ya kiungo fundi Amina Bilal katika kikosi cha timu yetu ya Simba Queens.
Amina ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa soka la Wanawake na amecheza timu tofauti nchini na msimu uliopita alikuwa akiitumikia JKT Queens na timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars.
Usajili wa Amina kwenye kikosi chetu unakuja kuongeza kitu kikubwa kuanzia kwenye michuano ya ndani hadi Kimataifa.
Msimu uliopita wa ligi Amina amefunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine sita (Assisti).
Kama ilivyokuwa kwenye timu ya wanaume hata Simba Queens tumefanya maboresho makubwa ya kikosi lengo likiwa kuandaa kikosi imara.
Katika msimu wa 2021/22 Amina alichaguliwa mchezaji bora Ligi (MVP) na msimu wa 2022/23 akachaguliwa katika kikosi bora cha msimu.