Karibu Simba, Pilsner Lager

Klabu yetu imeingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Serengeti Breweries kupitia bia yake ya Pilsner Lager.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema udhamini huu umekuja kuongeza kitu kikubwa sababu uendeshaji wa timu unagharimu kiasi kikubwa cha pesa.

Kajula amesema makubaliano haya yatakuwa na faida kwa pande zote huku aliwahakikishia Pilsner kurejea kwa kishindo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Tunawashukuru Serengeti kwa kudhamini huu, hamjakosea kutuamiani, mmekuja kwenye klabu sahihi. Tunaamini Muungano huu utakuwa na manufaa makubwa kwa pande zote mbili,” amesema Kajula.

Mkurugenzi Mkuu wa Serengeti Breweries, Obina Anyarebenchi amesema makubaliano ya leo lengo lake sio tu kukuza chapa ya Pilsner bali ni kuhakikisha Watanzania wanafurahia bia yao pendwa.

“Serengeti tunajivunia mkataba huu, hatujakuja Simba kwa bahati mbaya bali tunaujua ukubwa wa Simba na tunaamini utakuwa na faida kwetu pamoja na wenzetu,” amesema Obina.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Mjumbe wa Bodi Raphael Chegeni amesema Serengeti imewekeza sehemu sahihi na matunda yake wataanza kuyaona kuanzia sasa.

“Karibuni sana Serengeti Breweries, mmekuja sehemu sahihi wenye furaha. Simba ni timu kubwa na kwakuanzia Jumapili ya Novemba 5 mnataanza kupata furaha,” amesema Chegeni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER