Karibu Nyumbani Jentrix Shikangwa

Mshambuliaji nyota Jentrix Shikangwa amerejea katika kikosi cha Simba Queens kutoka Beijing Jingtan ya China baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Jentrix raia wa Kenya amerejea Simba Queens baada ya kupita miezi sita tu baada ya kujiunga na Jingtan Julai mwaka jana.

Wakati anaondoka kuelekea China, Jentrix alikuwa mfungaji bora Ligi Kuu ya Wanawake huku akifunga mabao 25.

Jentrix alijiunga nasi katika dirisha dogo la usajili Disemba mwaka 2022 na akacheza nusu msimu kabla ya kupata dili la China na sasa amerejea nyumbani.

Tunaamini uwezo wa Jentrix na kwa kusaidiana na wenzake aliowakuta tunaamini tutafanya vizuri na kurejesha mataji tuliyopoteza msimu uliopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER