Karaboue Chamou ni Mnyama

Tumefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi wa kati Karaboue Chamou raia wa Ivory Coast kutoka klabu ya Racing Club d’ Abidjan kwa mkataba wa miaka miwili.

Karaboue ana urefu wa futi 6.2 na yuko vizuri kwenye kucheza mipira ya juu kuzuia na kushambulia.

Moja ya eneo ambalo lilikuwa changamoto kubwa msimu uliopita ilikuwa ulinzi na ujio wa Karaboue ni moja ya tiba.

Karaboue anakuja kuongeza nguvu katika idara ya ulinzi wa kati ambapo atashirikiana na Che Fondoh Malone na Abdulrazack Mohamed Hamza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER