Kapombe: Tupo tayari asilimia 100

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe amesema kwa upande wao wachezaji wana utayari wa asilimia 100 kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa kesho Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kapombe amesema kila mchezaji atakayepewa nafasi ya kucheza atakuwa tayari kwa ajili ya kuipigania timu na kuwapa furaha Wanasimba na Watanzania.

Mlinzi huyo amewataka Watanzania na Wanasimba kuendelea kuwaamini kwani wamejipanga kuhakikisha wanawapa furaha kesho.

“Kikubwa ninachoweza kuwaambia Wanasimba na Watanzania kwa ujumla wawe na imani nasi, sisi wachezaji tumejipanga kuhakikisha tunawapa furaha.

“Tupo tayari kwa asilimia 100 na kila mchezaji morali ipo juu malengo yetu ni kuhakikisha tunapata tiketi ya kuingia hatua ya makundi Afrika kwa kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani,” amesema Kapombe.

Kapombe ameongeza kuwa tutaingia katika mchezo wa kesho bila kuangalia matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza kule Botswana na tutacheza kama ndiyo mara ya kwanza tunakutana ili kutafuta ushindi na hatimaye tuingie hatua ya makundi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER