Kapombe, Sakho, Banda wachuana mchezaji bora Machi

Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao ni mlinzi wa kulia Shomari Kapombe, kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho na winga Peter Banda.

Walinzi wa kati Joash Onyango na Henock Inonga waliingia katika tano bora lakini baada ya mchujo wamebaki Kapombe, Sakho na Banda.

Ndani ya mwezi Machi tumecheza mechi nne ambapo Kapombe amecheza tatu na kutoa assist mbili. Sakho amecheza mechi nne akifunga mabao mawili na assist moja. Banda yeye amecheza mechi nne hajafunga lakini akisaidia kupatikana kwa bao moja.

Mshindi atapatikana baada ya kupigiwa kura nyingi kutoka kwa mashabiki kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz

Zoezi la kupiga kura litaanza leo saa 10 jioni mpaka Machi 27 ambapo mshindi atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

SHARE :
Facebook
Twitter

68 Responses

  1. I love peter banda he is inspire me .He is my model and to my side he is young and good player at his age i would like to see him playing in UEFA OR PRIMEAR LEAGUE

  2. I love peter banda he is inspire me as my model i would like to see him playing in UEFA or PRIMIER LEAGUE keep it up good work you are still young and super taleted

  3. Simba is a big Club please try to use English or both English and Swahili….It’s a big Club,we respect it so much

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER