Kapombe: Naendelea vizuri namshukuru Mungu

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe amesema hali yake kwa sasa inaendelea vizuri na kesho ataenda hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Kapombe alipata maumivu ya mguu katika mchezo wetu wa kwanza wa ligi dhidi ya Biashara United yaliyomfanya kukosa mechi iliyofuata ya Dodoma Jiji.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri hali yangu iko poa na kesho nitaenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi,” amesema Kapombe.

Kutokana na majeraha hayo, Kapombe ameenguliwa kwenye kikosi cha Timu ya Tanzania (Taifa Stars) kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia utakaopigwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER