Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe ndiye mchezaji pekee kati ya 23 waliopo kikosini ambaye atakosekana katika mchezo wa pili wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa kesho Uwanja wa Jamhuri saa 10 jioni.
Kapombe aliumia katika mchezo wetu wa kwanza wa ligi dhidi ya Biashara United ambapo alishindwa kuendelea na mechi kipindi cha pili akafanyiwa mabadiliko.
Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema ukimuacha Kapombe wachezaji wengine wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho ambao tunaamini utakuwa mgumu.
“Tunahitaji alama tatu kwenye mchezo wa kesho kutokana na matokeo ya mechi zetu tatu za zilizopita ili kurudisha ari kikosini pamoja imani na hamasa kwa mashabiki.
“Maandalizi yamekamilika wachezaji wako tayari isipokuwa tutamkosa Kapombe kutokana na kuwa majeruhi. Tunafahamu ligi ni ngumu hasa mechi za ugenini kutokana na aina za viwanja lakini tupo kamili na lengo ni moja kupata alama tatu,” amesema Matola.